fbpx

Kuhusu

AFYA Colleges

AFYAColleges ni jukwaa la elimu lililobuniwa kusaidia wanafunzi kufikia malengo yao ya kuwa wataalamu bora wa afya na kuwa na maisha mazuri baada ya masomo.

Tumejitolea kutoa ushauri, msaada, na huduma kwa wanafunzi katika kuchagua kozi za afya, kupata vyuo bora, kupata vifaa vya mafunzo, na kuunganisha wanafunzi na fursa za kazi baada ya masomo.

Picha ya Dr. Adinan_AFYAColleges_AFYATech CEO

“Mafanikio yako ya kesho ni hatua tunazochukua leo. AFYAColleges iko hapa kukusaidia kufikia ndoto zako!” 

Dr. Adinan J. — CEO AFYATech
Mchango wa AFYAColleges Kwa Ufupi

0
K+
Tumewafikia
0
+
Wataalamu
0
+
Michango
0
+
Kuunganishwa Vyuo

Maono Yetu

ni kuwa jukwaa kuu la kusaidia wanafunzi kufikia mafanikio yao katika uwanja wa afya. Tunataka kuwa mwongozo wako na rasilimali muhimu katika safari yako ya elimu ya afya, na kuhakikisha unapata elimu bora, vifaa vya hali ya juu, na fursa nyingi za kazi katika sekta ya afya.

Dhamira Yetu

ni kukuwezesha kufikia ndoto yako ya kuwa mtaalamu bora wa afya. Tuna lengo la kukupa ushauri sahihi na thabiti kuhusu kozi za afya, kukusaidia kupata vyuo bora vinavyolingana na mahitaji yako, na kukupa vifaa vyenye ubora wa juu kwa ajili ya mafunzo yako. Baada ya kumaliza masomo, tunakusudia kukushauri kuhusu fursa zilizopo na kukusaidia kutambua njia bora ya kuzitumia.

Tunaamini

kuwa kila mwanafunzi anayo uwezo wa kufikia malengo yake katika fani ya afya. Tunaamini katika kuwezesha na kutoa rasilimali sahihi ili kila mwanafunzi aweze kufikia uwezo wake kamili na kuchangia katika kuboresha huduma za afya katika jamii.

Shopping Basket