fbpx

Fursa zilizopo baada ya kuhitimu masomo ya afya

Fursa Zitokanazo na Kusoma Kozi Za Afya

Unaweza kuniambia kozi gani inalipa? Nawe unajiuliza kozi ipi inalipa?

Kama bado hujajiuliza huwenda ukaulizwa baadae. Nimekuwa nikiulizwa sana hili swali na wengi wanaotaka kujiunga kusoma kozi za afya na hata wale wanaopanga kujiendeleza kimasomo baada ya kuhitimu ngazi moja.

Kwamfano, nimekuwa nikiulizwa na madaktari wanaotaka kusoma zaidi na kuwa bingwa. Hili swali nimelijibu kinagaubaga sehemu ingine.

Ila kwa muhtasari, nilichosema kule, ni kwamba kozi zote zinalipa!

Je, fursa ni zipi baada ya kuhitimu mafunzo ya uuguzi, kwa mfano?. Kulingana na ngazi yako fursa ziko nyingi sana.

Tukumbuke fani ya afya imegawanyika katika makundi mbalimbali kuanzia kutoa huduma mpaka biashara.

Kwa kutaja kazi chache, kuna kupata ujira kutokana na

  1. kuhudumia wagonjwa katika vituo vya afya,
  2. kufundisha katika vyuo mbalimbali vya afya,
  3. kufanya kazi katika utafiti,
  4. kufanya kazi katika makampuni ya madawa,
  5. Kufanya kazi katika makampuni ya vifaa vya hospitali, pia
  6. unaweza kufanya kazi kama mshauri au
  7. Kufanya katika miradi mingine ya afya katika taasisi mbali mbali za afya kama wizara za afya, WHO na mashirika mengine kama hayo.

Fursa zote hizi zilizoko kwa waliofanya kozi za afya / wataalamu wa masuala ya afya yapo katika mazingira yetu na kwingineko popote duniani kwani uhitaji wa wataalamu hawa ni mkubwa mno.

Na hata serikali inapochelewa kutangaza ajira haimaanishi hawahitajiki / au wametosha. La hasha! Ni kutokana na ufinyu wa bajeti. 

Shopping Basket