Kozi za Afya Tanzania 2026: Sifa, Ada, na Vigezo vya Kujiunga (NACTVET)

Kozi za afya zimegawanyika katika makundi mawili makubwa:

  1. Masomo ya Kliniki (Clinical): Huusisha uhusiano wa moja kwa moja kati ya mgonjwa na daktari au muuguzi.
  2. Yanayosaidia Matibabu (Allied Health Sciences): Husaidia katika utambuzi na matibabu ya magonjwa.

Usipofahamu makundi haya na vigezo vyake, unaweza kukata tamaa ukifikiri umekosa sifa, au ukachagua kozi isiyoendana na ufaulu wako. Mwaka jana na mwaka huu, kupitia CollegePlan (huduma yetu ya ushauri), tumesaidia wanafunzi zaidi ya 50 waliokuwa wamekosea kuchagua kozi kutokana na kukosa taarifa sahihi.

Kuchagua kozi ya afya ni moja ya maamuzi makubwa zaidi katika maisha ya mwanafunzi. Swali ambalo nimekuwa nikiulizwa kila siku ni: “Je, nina sifa za kujiunga na chuo cha afya?” au “Ni kozi gani ya afya inanilipa?”

Mwongozo huu utakuonyesha orodha ya kozi za afya zinazotolewa nchini, vyuo vinavyofundisha, vigezo vya NACTVET, na ada zao.


Jedwali la Sifa na Ada za Kozi za Afya 2026

Hapa kuna muhtasari wa haraka wa sifa za kujiunga na vyuo vya afya vya serikali na binafsi. Hii itakusaidia kufahamu kama unakidhi vigezo kabla ya kuanza maombi.

Jina la Kozi (Health Course)Sifa za Kujiunga (CSEE)Muda wa MasomoKadirio la Ada (Serikali)
Clinical Medicine (Utabibu)Alama D ya Bio, Chem, Phys na somo 1 lingine.Miaka 3Tsh 900,000 – 1,200,000
Nursing & Midwifery (Uuguzi)Alama D ya Bio, Chem, Phys na somo 1 lingine.Miaka 3Tsh 900,000 – 1,500,000
Environmental HealthAlama C ya masomo 3 (ikiwemo Hesabu).Miaka 3Tsh 900,000 – 1,200,000
Pharmaceutical Sciences (Famasia)Alama D ya Bio, Chem, Phys na somo 1 lingine.Miaka 3Tsh 1,000,000 – 1,500,000
Medical Laboratory (Maabara)Alama D ya Bio, Chem, Phys na somo 1 lingine.Miaka 3Tsh 1,000,000 – 1,400,000

Makundi ya Kada na Kozi za Afya

1. Kozi ya Utabibu (Clinical Medicine)

Hawa ndio wataalamu maarufu tunaowaita madaktari. Kazi yao ni kufahamu magonjwa, kuyachunguza, na kuyatibu. Ikiwa unatafuta sifa za kujiunga na vyuo vya afya vya serikali kwa ngazi ya diploma, Clinical Medicine ndiyo kozi inayoshika nafasi ya kwanza kwa ushindani.

Kozi ya clinical medicine hutoa wataalamu wa afya kama wailio hapa chumba cha upasuaji, co, doctor
kozi ya uuguzi-nursing-sifa-vyuo-ada-mob-AFYAColleges

2. Kozi ya Uuguzi (Nursing & Midwifery)

Wauguzi ndio wanaokaa na mgonjwa kwa muda mrefu zaidi. Kazi yao ni kuhakikisha mgonjwa anapata dawa na huduma zote muhimu. Kwa wanaotaka kusoma visiwani, unaweza kuangalia sifa za kujiunga na chuo cha afya Mbweni Zanzibar.

3. Kozi ya Environmental Health Science (Bwana Afya)

Wataalamu hawa huhakikisha mazingira yanakuwa salama ili kuzuia magonjwa.

heart, love, nature, chalcedony, light blue, happiness, stone, bio, pesticides, health, outdoors, natural reserve, environmental protection, chalcedony, chalcedony, chalcedony, chalcedony, chalcedony, pesticides
Focused businesswoman holding cup, analyzing financial data at desk.

4. Ukatibu wa Afya (Health Secretary)

Hii ni kozi kwa wale wanaopenda usimamizi wa taarifa za afya na utawala. Inahitaji umakini mkubwa katika kutunza siri za wagonjwa na takwimu.

5. Kozi ya Famasia na Maabara

Kozi hizi ni muhimu kwa utambuzi wa magonjwa (Maabara) na utoaji wa dawa sahihi (Famasia). Zote zinahitaji ufaulu wa kuanzia Alama D katika masomo ya sayansi.

Two adults exploring medicine options at a pharmacy in Lagos, Nigeria.

Ada za Vyuo vya Afya vya Serikali 2026

Moja ya changamoto kubwa kwa wanafunzi ni gharama. Ikiwa unatafuta ada za vyuo vya afya vya serikali, wastani wake ni kati ya Tsh 900,000 hadi Tsh 1,500,000 kwa mwaka kwa ngazi ya Diploma. Vyuo vya binafsi vinaweza kutoza kati ya Tsh 1,800,000 na kuendelea.


Unahitaji Msaada wa Kuchagua Kozi?

Usikubali kupoteza nafasi yako kwa kukosea kuchagua kozi isiyoendana na ufaulu wako. Huduma yetu ya CollegePlan ipo hapa kukusaidia kuanzia mwanzo wa maombi hadi unapopata chuo.

[BONYEZA HAPA KUPATA USHAURI WA COLLEGEPLAN]

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

Naweza kusoma kozi za afya kama sina physics / fizikia?

Kwa kozi nyingi za kitabibu (Nursing, Clinical Medicine), Fizikia ni lazima iwe angalau Alama D. Hata hivyo, baadhi ya kozi za utawala wa afya zinaweza kuwa na vigezo nafuu zaidi.

Vyuo gani vya serikali vina ada nafuu?

Vyuo vingi vya serikali vilivyopo chini ya Wizara ya Afya na TAMISEMI vina ada inayofanana na hupangwa kwa mujibu wa miongozo ya serikali.

What’s Included in Your Packages?

Our travel packages typically include accommodation, transportation, and some guided tours. Check the details to see what’s specifically covered for each package.


error: Content is protected !!
Scroll to Top
0

Subtotal