fbpx
green and yellow plant on white wooden fence

Kozi za Afya Zenye Soko ni Zipi: Jitume Kuongeza Kipato

Koziza afya zenye soko zaidi ni zipi? Hili ni swali ambalo nimekuwa nikilijibu mara nyingi sana.

Wanafunzi wenye uchu wa maendeleo wamekuwa wakiuliza. kwahiyo kama una swali hili kichwani usifikiri kwamba wewe ni mbinafsi.

Kwamba wewew unapenda sana pesa kulikko kutoa huduma. Kuwa na amani. Uko sawa. Kwanini nakwambia uko sawa?

Soma Kozi Bora kwenye Chuo Bora!

Pata muongozo kutoka kwa Dr. Adinan. Jiunge na waliofanikiwa kwa kusoma kitabu hiki. Jaza fomu hii kama ungependa ushauri kutoka kwa Dr. Adinan

Una haki ya kujua utapata kipato gani kwa kazi unayoifanya na kazi ipi itakupatia kipato kikubwa utakachoweza kuendesha maisha yako vizuri. 

Huitaji kuwa jasusi kufahamu kwamba maelfu ya watanzania wanafunzi wamekuwa wakisumbuka kwenye mashule, vyuo mbalimbali kwasababu ya kukosa ada.

Kwani ada ni nini? Ni pesa. Ndio ni pesa. Kwahiyo kama tunakubaliana elimu ni mhimu, pia ada nayo ni muhimu. Pesa ni muhimu vilevile. Umeona?

Kama mtaalamu wa afya wa baadae inakubidi kufahamu wapi uwekeze ili upate kiwango kizuri cha pesa.

Huna tofauti na wanaouliza wafanye biashara gani kujiongezea kipato au kupata kipato kikubwa. 

Wakati huu wewe nimwanataaluma, si vizuri tu, bali ni lazima kujua kozi inayolipa.

Ninakufahamisha kanuni.

Kozi ipi ya afya inalipa zaidi?

Kujibu swali hili naomba nikupigie hadithi moja.

Mzee Musa, mkulima mmoja akimuhadithia menzake, Mzee Lema kuhusu kiwango cha magunia anayopata kutoka kwenye shamba lake la mpunga, alisema yafuatayo.

Sasa hivi napata gunia 100 kutoka kwenye hekari tano. Mzee Lema alishangaa akamwambia mbona mimi napata gunia hizo hizo kwenye kwenye hekari 10? Na nina pembejeo kama vile trekta?

Mzee Musa kamwambia mzee Lema, hakuna mchawi. Ni mbinu za ukulima bora. Naeza fahamu mbegu unayotumia na mbolea?

Mzee Lema kamuonesha, hii hapa. Mzee Musa akamwambia, sisi tumepewa mbegu hizi na tunapanda kwa umbali huu.

Tangu wataalamu wamekuja kutufundisha mbinu hizi, tunapiga pesa mbaya!

Hii inafanana na malipo kutokana na kazi. Tufahamu kwamba malipo yanatokana na wewe mwenyewe, unpofanyia kazi na kazi yako mwenyewe.

Elimu ni nyenzo kama lilivyokuwa terekta kwa mkulima anayepata mavuno madogo, mzee Lema. Wote wawili ni wakulima, ila mzee Musa kamzidi mzee Lema mbinu.

Kote nilipofanya kazi nimekutanan na fani zote. Kuanzia mfagiaji, mhazili/secretary mpaka wenye PhD.

Ni kuhakikishe kwamba elimu uliyonayo haitakuacha bila kipato. Lakini kuifanya ikupe kipato kikubwa ni wewe mwenyewe. na kuifanya ikupe kipato kidogo ni wewe mwenyewe. Sikiliza sauti hii kukuza kipato kutumia elimu yako ya afya uliyoipata.

Sikiliza Ushauri Huu

Fursa Zitokanazo na Kusoma Kozi Za Afya

Unaweza kuniambia kozi gani inayolipa? Nawe unajiuliza kozi ipi inalipa?

Kama bado hujajiuliza huwenda ukaulizwa baadae. Nimekuwa nikiulizwa sana hili swali na wengi wanaotaka kujiunga kusoma kozi za afya na hata wale wanaopanga kujiendeleza kimasomo baada ya kuhitimu ngazi moja.

Kwamfano, nimekuwa nikiulizwa na madaktari wanaotaka kusoma zaidi na kuwa bingwa. Hili swali nimelijibu kinagaubaga sehemu ingine.

Ila kwa muhtasari, nilichosema kule, ni kwamba kozi zote zinalipa!

Je, fursa ni zipi baada ya kuhitimu mafunzo ya uuguzi, kwa mfano?. Kulingana na ngazi yako fursa ziko nyingi sana.

Tukumbuke fani ya afya imegawanyika katika makundi mbalimbali kuanzia kutoa huduma mpaka biashara. Kwa kutaja kazi chache, kuna kupata ujira kutokana na

  1. kuhudumia wagonjwa katika vituo vya afya,

  2. kufundisha katika vyuo mbalimbali vya afya,

  3. kufanya kazi katika utafiti,

  4. kufanya kazi katika makampuni ya madawa,

  5. Kufanya kazi katika makampuni ya vifaa vya hospitali, pia

  6. unaweza kufanya kazi kama mshauri au

  7. Kufanya katika miradi mingine ya afya katika taasisi mbali mbali za afya kama wizara za afya, WHO na mashirika mengine kama hayo.

Fursa zote hizi zilizoko kwa waliofanya kozi za afya / wataalamu wa masuala ya afya yapo katika mazingira yetu na kwingineko popote duniani kwani uhitaji wa wataalamu hawa ni mkubwa mno.

Na hata serikali inapochelewa kutangaza ajira haimaanishi hawahitajiki / au wametosha. La hasha! Ni kutokana na ufinyu wa bajeti

Kozi za afya zenye ajira ya haraka

Katika ulimwengu wa leo, elimu ni muhimu sana katika kufikia mafanikio. Hata hivyo, ni muhimu pia kufahamu kwamba elimu pekee haiwezi kuhakikisha mafanikio ya kifedha.

Inahitaji kujituma na kuongeza soko lako katika eneo lako la kazi. Kwa wale wanaopenda kufanya kazi katika sekta ya afya, kuna kozi kadhaa ambazo zina soko kubwa na zinaweza kukusaidia kuongeza kipato chako.

Radiology

Kozi ya radiolojia ni moja ya kozi ambazo zina soko kubwa katika sekta ya afya. Radiolojia ni uwanja unaohusika na utambuzi na matibabu ya magonjwa kwa kutumia mionzi.

Kwa kuwa teknolojia ya mionzi inaendelea kukua, kuna mahitaji makubwa ya wataalamu wa radiolojia. Kwa kufanya kozi hii, utakuwa na fursa nzuri ya kupata ajira katika hospitali, vituo vya matibabu, na maeneo mengine ya huduma za afya.

Anesthesia

Kozi ya anesthesia ni nyingine ambayo ina soko kubwa katika sekta ya afya. Wataalamu wa anesthesia wanahusika na kutoa huduma za kupunguza maumivu wakati wa upasuaji au taratibu nyingine za matibabu.

Kazi hii inahitaji ujuzi mkubwa na umakini, na kuna uhaba mkubwa wa wataalamu wa anesthesia katika maeneo mengi. Kwa kufanya kozi hii, utakuwa na fursa ya kufanya kazi katika hospitali, vituo vya upasuaji, na kliniki za matibabu.

Health Information Sciences

Kozi ya sayansi ya taarifa za afya ni nyingine ambayo ina soko kubwa. Wataalamu wa sayansi ya taarifa za afya wanahusika na usimamizi na uchambuzi wa taarifa za afya.

Wanahitaji kuwa na ujuzi katika teknolojia ya habari na mifumo ya kumbukumbu za afya. Kwa kuwa teknolojia ya habari inaendelea kukua katika sekta ya afya, kuna mahitaji makubwa ya wataalamu wa sayansi ya taarifa za afya.

Kwa kufanya kozi hii, utakuwa na fursa ya kufanya kazi katika hospitali, vituo vya afya, na makampuni ya teknolojia ya afya.

Kwa kumalizia, ni muhimu kutambua kwamba kujituma na kuongeza soko lako ni muhimu sana katika kufikia mafanikio ya kifedha katika sekta ya afya.

Kozi za afya zenye soko kubwa kama radiology, anesthesia, na sayansi ya taarifa za afya zinaweza kukusaidia kuongeza kipato chako na kufikia malengo yako ya kazi.

Chagua kozi ambayo inakuvutia na ambayo inakidhi maslahi yako, na ujitume katika kujifunza na kuendeleza ujuzi wako. Kumbuka, elimu ni muhimu, lakini inahitaji kujituma ili kuwa na mafanikio ya kifedha katika sekta ya afya.

Tukusaidie kufanikisha maombi ya chuo?

Jaza fomu kuwasiliana na Dr. Adinan. Utalipia TSh. 9,000/ Tu!