fbpx

Monofilament

Sh19,900.0

Monofilament ni kifaa wagonjwa wa kisukari wanachotumia ili kujikinga na vidonda vya miguu kwa kufahamu viashiria mapema. Monofilament inakufahamisha kama miguu yako inahisi vizuri – utimamu wa mishipa ya fahamu.

Kama una kisukari kifaa hichi kitakufaa. Kwasababu kisukari huaribu mishipa ya fahamu hivyo hukuweka hatarini kupata vidonda hasa miguuni.

Kwa kutumia kifaa hichi unaweza kufahamu hali yako ya mishipa ya fahamu kwa uhakika na kuweza kuchukua hatua stahiki kwa haraka ikiwemo kubadilisha tiba.

Availability: 229 in stock

Faida: Ishi na kisukari bila hofu ya kupata vidonda miguuni.

Vidonda kwa wagonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa sana inayosababisha ulemavu unaotokana eidha kwa kukatwa miguu au mikono. Haya yote yanaweza kudhibitika kama tahadhari itachukuliwa katika muda muafaka. Hatahivyo, wengi wa wagonjwa wa kisukari hawajui.

Sukari husababishaje Vidonda? Sukari inatakiwa ihifadhiwe kwenye tishu, isikae ndani ya damu. Inapokaa kwenye damu kwa kiwango kikubwa husababisha sumu inayofanya uharibifu kwa namna tatu.

1. Kwanza huaribu mishipa ya fahamu na hivyo hutoweza kuhisi. Ukosefu wa hisia husababisha mwenye kisukari kutokufahamu kama mguu unaumia-mkandamizo kwamfano kubanwa na kiatu nk.

2.  Kisukari pia huaribu mishipa ya damu na -kama tulivyoona- kusababisha hali inayoitwa artherosclerosis. Hatimaye mishipa ya damu huziba haswa ile ya pembeni ya mwili kama vile miguu. Kukosekana kwa damu maana yake sehemu husika hukosa chakula, hewa safi na kinga. Hivyo sehemu hiyo hufa na kama utapata maambukizi hutapona kwa urahisi. Mara nyingi hii imekuwa sababu kubwa ya wagonjwa wa kisukari kukatwa miguu.

3.  Njia ya tatu, sukari huathiri kinga ya mwili kwa kuharibu na kupunguza muda wa kuishi wa seli zinazopambana na magonjwa.

Suluhisho: Kifaa hichi kitakusaidia kufahamu utimamu wa mishipa yako ya fahamu pamoja na kama bado una hisia kwenye miguu. Hivyo kifaa hichi kitakusaidia katika kujikinga na vidonda vya kisukari kwa kufanya yafuatayo. Kwa kuhakikisha unapambana kushusha sukari ukiwa na uhakika wa kiwango unachotaka kukishusha na kufahamu hali yako ya hisia kwenye miguu. Haya yote yatakuongezea ufahamu na hivyo kuchukua hatua stahiki.

Reviews

There are no reviews yet.

Only logged in customers who have purchased this product may leave a review.