fbpx

Mikopo kwa Wanafunzi wa Vyuo

Maelekezo Muhimu kwa Wanafunzi Wote Wanaoomba Mikopo

Mikopo ya elimu kwa ngazi ya Diploma / Stashahada hutolewa na Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa miongozo. Kwa mwaka wa masomo 2023/2024 muongozo ulitoa mazingatio yafuatayo:

Soma Kozi Bora kwenye Chuo Bora!

Pata muongozo kutoka kwa Dr. Adinan. Jiunge na waliofanikiwa kwa kusoma kitabu hiki. Jaza fomu hii kama ungependa ushauri kutoka kwa Dr. Adinan

  1. Kusoma na kufuata taratibu za maombi katika Mwongozo wa mwaka wa masomo 2023/2024.


  2. Kuhakikisha kuwa namba ya mtihani wa kidato cha nne atakayoitumia mwombaji iwe sawa na atakayoombea udahili wa chuo.


  3. Kuhakikisha kuwa fomu ya maombi ya mkopo na mkataba zimesainiwa na viongozi wa serikali ya mtaa, mdhamini na kamishna wa viapo.


  4. Waombaji wajaze fomu zao kwa ukamilifu na kuzisaini kabla ya kuziwasilisha HESLB kwa njia ya mtandao.


  5. Kuhakikisha kwamba vyeti vya kuzaliwa/vifo vimethibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) au Afisa aliyeteuliwa ili kuthibitisha uhalali wa nyaraka hizo.


  6. Kwa mwombaji mwenye taarifa zake za benki ajaze kwa usahihi kwenye fomu ya maombi ya mkopo.


  7. Kwa mwombaji mwenye Namba ya simu na kitambulisho cha taifa (NIDA) ahakikishe anajaza namba hizo wakati wa kuomba mkopo.


  8. Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa mwisho wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao.

Kufunguliwa Dirisha la Maombi

Kwa wanafunzi wa mwaka jana kuomba mikopo ya elimu kwa ngazi ya Stashahada, dirisha la maombi ya mkopo kwa mwaka wa masomo 2023/2024 lilifunguliwa kuanzia tarehe 07 Oktoba, 2023 hadi tarehe 22 Oktoba, 2023.

Programu za Kipaumbele kwenye Afya na Sayansi Shirikishi

Mikopo hii kwa kozi za diploma au kama wengi wanvyopenda kuviita vyuo vya kati hubadilika kulingana na uhitaji wa nchi kwa wakati husika.

Kwa mfano, kwa mwaka wa masomo 2023/2024, mikopo itatolewa kwa wanafunzi waliodahiliwa katika Programu/Stashahada zinazoangukia katika maeneo sita ya kipaumbele.

Kozi za afya zilizopewa kipaumbele mwaka 2023/2024 zinajumuisha:

  1. Clinical Dentistry
  2. Diagnostic Radiotherapy
  3. Occupational Therapy
  4. Physiotherapy
  5. Clinical Optometry
  6. Dental Laboratory Technology
  7. Orthotics & Prosthetics
  8. Health Record & Information
  9. Electrical and Biomedical Engineering
 
 

Sifa Stahiki za Kupata Mkopo kwa Kozi za Diploma

Sheria na Kanuni za Bodi ya Mikopo zinaainisha sifa na vigezo vya jumla kwa wanafunzi wanaohitaji mkopo baada ya kudahiliwa na vyuo vyenye ithibati. Mwombaji atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

Vigezo vya Kupata Mkopo Ngazi ya Diploma

  1. Awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 27 wakati wa kuomba mkopo.


  2. Awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu inayotoa elimu ya ngazi ya kati nchini.


  3. Awe amekamilisha na kuwasilisha maombi ya mkopo kupitia mfumo wa maombi ya mkopo (OLAMS).


  4. Asiwe na ajira au mkataba wa kazi wa serikalini au sekta binafsi unaompatia mshahara au kipato.


  5. Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne (CSEE), Cheti (astashahada) au kidato cha sita (ACSEE) au ndani ya miaka mitano; yaani kati ya mwaka 2019 hadi 2023.

Hali ya Kijamii na Kiuchumi

Mwombaji anaweza pia kustahiki mkopo kulingana na hali yake ya kijamii na kiuchumi. Hali zinazostahiki ni:

  1. Uyatima; aliyefiwa na mzazi au wazazi.


  2. Familia au kaya ya kipato duni inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) au taasisi nyingine za kitaifa zinazotoa ufadhili kwa kaya zenye vipato duni.


  3. Ulemavu wa mwombaji au wazazi wake.

Upangaji wa Mikopo

Upangaji wa mikopo utazingatia vipaumbele vifuatavyo:

  1. Mwanafunzi mwenye udahili kwenye programu za vipaumbele vya Taifa kama zilivyofafanuliwa katika Mwongozo huu zitazingatiwa.


  2. Ufaulu wa kitaaluma uliomuwezesha kudahiliwa kwa ajili ya elimu ya ngazi ya kati.


  3. Hali ya kijamii kama ilivyofafanuliwa katika mwongozo huu.

Nyaraka za Kuambatisha Wakati wa Maombi ya Mkopo

Zifuatazo ni nyaraka muhimu za kuambatisha kwenye maombi ya mkopo:

  1. Cheti cha kuzaliwa kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji kutoka Zanzibar au namba ya uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara.


  2. Vyeti vya vifo vya wazazi kuthibitisha uyatima kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji kutoka Zanzibar au namba ya uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara.


  3. Fomu ya kuthibitisha Ulemavu wa mwombaji au mzazi iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mkoa (RMO).


  4. Fomu ya kuthibitisha Ulemavu wa mzazi wa mwombaji iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO).

Katika mwaka wa masomo 2023/2024, mikopo itatolewa kwa wanafunzi waliodahiliwa katika Program/Stashahada zinazoangukia/zilizomo katika maeneo sita ya kipaumbele yaliyoidhinishwa.

Naombaje Mkopo?

Kuomba mkopo kusoma kozi ya diploma inaomba HESLB. Mwanafunzi inabidi aingie kwenye tovuti ya HESLB kujaza taarifa zake. Bonyeza HAPA Kuomba mkopo

Tunakutakia kila la kheri katika maombi yako ya mkopo wa elimu!