Kozi za afya, moja ya eneo muhimu sana mwanafunzi inabidi afahamu. Mwaka jana na mwaka huu kupitia CollegePlan, huduma yetu ya ushauri na msaada kwa wanafunzi tumesaidia wanafunzi zaidi ya 50 waliokosea kuchagua kozi.
Wanafunzi wengi wanakosea kuchagua kozi kwasababu hawazijui. Wanafunzi wengi wanafahamu kozi za afya kupitia kwa wenzao.
Ungependa kufahamu kuhusu kozi za afya: orodha ya kozi zinazotolewa nchini, vyuo vinavyofundisha, vigezo na sifa za kujiunga na ada zao uko sehemu sahihi? Uko sehemu sahihi.
Soma Kozi Bora kwenye Chuo Bora!
Pata muongozo kutoka kwa Dr. Adinan. Jiunge na waliofanikiwa kwa kusoma kitabu hiki. Jaza fomu hii kama ungependa ushauri kutoka kwa Dr. Adinan
Orodha ya Kada na Kozi Za Afya
Ingawa watu wengi wakiwa wanawafahamu daktari na muguzi kama watoa huduma ya afya, kuna wahudumu wengi wengine ambao huchangia kutoa huduma ya afya katika sekta hii muhimu.
Kada za afya ni kama nilivyoainisha hapa chini. Hatahivyo, ni muhimu kufahamu kwamba orodha hii imekusanya zile kada kubwa kwahiyo zingine zinaweza kukosekana. Hizi tutaziongeza kadri tutakvyoona inafaa.
1. Kozi ya Radiologia:
Kozi ya radiology Ulishawahi kusikia X-Rays na ultrasound? Hivi ni vipimo muhimu ambavyo hutumika kufahamu ugonjwa wa mteja au kufahamu maendeleo yake.
Wataalamu wa radiolojia kimsingi wanapima kwa kuona picha ya sehemu husika.
Kwamfano hutumia XRay kuangalia mapafu na kufahamu kama una pneumonia au kuangalia mfupa na kujua kama umevunjika.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo matatu (3) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi.
2.Kozi ya Maabara (Laboratory sciences):
Kozi hii ya maabara itakupa utaalamu wa kuweza kutumia vifaa na vipimo maalum kubaini maradhi, aina za chembechembe katika mwili ambazo hazionekani kwa macho.
Wataalamu wa maabara wamekuwa kiungo muhimu sana kati ya mgonjwa na tabibu.
Kwani bila kufahamu aina ya ugonjwa au baadhi ya hali ya kemikali mwilini zilivyo tiba haiwezi kutendeka kwa ufanisi.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
3. Kozi ya Tiba kwa njia ya mazoezi (Physiotherapy):
Physiotherapia ni fani ya tiba kwa njia ya mazoezi ili kurudisha utendaji kazi wa viungo baada ya upasuaji au baada ya ajali au kuumwa magonjwa ya aina ingine kwa mdua mrefu.
Kwasasa hali ilivyo, watu wengi sana wanasumbuliwa na maumivu ya mgongo. Wataalamu hawa wa physiotherapia wanaweza kuwatibu kwa haraka bila hata kuhitaji dawa au upasuaji.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
4. Kozi ya Tiba kwa njia ya kazi (Occupational therapy):
Hii ni fani itakayokupa ujuzi kumsaidia mteja wako kuweza kufanya kazi baada ya ulemavu uliotakana na maumbile wakati wa kuzaliwa au ajali.
Wataalamu hawa huzingatia kwa umakini uwezo na kutumia kile ulichonacho sasa kuboresha maisha ya mteja kuliko kila ambacho hana.
Ulishawahi kuona watu wasiokuwa na mikono wanaandika kwa mguu? Wataalamu wa ocuupational therapy wanaweza kukufundisha kufanya hivi.
Mfano mwengine ni wale watoto wanaozaliwa na mtindio wa ubongo na kutokuweza kutembea, wataalamu hawa huweza kuwasaidia kutembea kwa kiwango ambacho ubongo utakuwa umeathirika.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikijumuisha C kupita katika Biolojia na masomo yoyote mawili ya Kemia, Hisabati, Jiografia, Uchumi, Fizikia/Sayansi ya Fizikia.
5. Kozi ya Ufamasia / Madawa (Pharmaceutical sciences):
Hii ni moja ya fani ambazo tumekuwa tukiwaona wataalamu wake mara kwa mara.
Wafamasia kwa ufupi tunasema ni wale wanaokupatia dawa hospitali pale unapoambiwa na daktari nenda kwenye dirisha la dawa au hata katika maduka ya dawa.
Kutoa dawa ni kazi moja na huwenda ndiyo ndogo kabisa kwa taaluma hii. Taaluma yao huwawezesha pia kutengeneza dawa, kuchanganya dawa, kusimamia uhifadhi na usambazaji wa dawa pia.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
6. Kozi Uhandisi wa vifaatiba / vipimo (Biomedical engineering):
Biomedical engineering ni kozi itakayokuwezesha kutengeneza, kudizaini na kufanyia marekebisho vifaatiba vinavyotumika katika vituo vya afya.
Wengine watasema hii ni kozi ya uhandisi. Mimi nimeiweka hapa kama kozi ya afya kwasababu ya umuhimu wake wa moja kwa moja katika kutoa huduma ya afya na tiba.
Soma zaidi kufahamu vyuo, sifa na vigezo vya kujiunga, vyuo na ada zake kwa kubonyeza hapa
7. Kozi ya Ufundi wa viungo bandia (Prosthetics and orthotics):
Wakati mwengine binadamu hupata ajali na kupoteza kiungo au viungo katika mwili.
Wengi wetu tumeshaona watu wakiwa na mikono, miguu au masikio bandia.
Vifaa bandia hivi hutengenezwa kwa makusudio maalum, kurudisha kazi na muonekano – kupendezesha.
Umekumbuka story ya jicho la kondoo? Watu waliopoteza macho huwekewa jicho la bandia ili kumfanya awe na muonekano kama aliokuwanao kabla ya kupata ajali.
Unaweza kupata taarifa za kina kwa kutembelea website ya chuo cha viungo bandia KCMC.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulualama C katika masomo matatu (3) kutoka Fizikia, Kemia, Baiolojia au Hisabati. Ufaulu wa C katika masomo ya Uhandisi pia unakubalika
8. Kozi ya Utabibu / udaktari (Medicine):
Clinical Medicine, tabibu ni maarufu. Hawa ndiyo wale tunaowaita madaktari. Kazi yao ni kufahamu magonjwa, kuweza kuyachunguza na kuyatibu.
Wako madaktari wa ngazi mbalimbali-diploma (clinical medicine au clinical officer), stashahada ya juu (AMO), shahada (Medical Doctor) na daktari bingwa (specialist).
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
9. Kozi ya Uuguzi / Unesi (Nursing):
Wauguzi husaidiana na matabibu kutoa huduma kwa mgonjwa. Moja ya kazi za wauguzi ni kuhakikisha mgonjwa kapata dawa, kafanyiwa procedures au vipimo ambavyo ilielekezwa.
Hospitali huwa tunasema kwamba wagonjwa wote ni wa wauguzi kwani huwa nao muda mwingi kuliko mtaalamu mwengine yeyote wa afya.
Kwa wajawazito, kama muuguzi utahitaji kupima ukuaji wa mimba, kumtaarifu tarehe ya kujifungua, na kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto na kumzalisha pindi muda ukifika.
Bonyeza HAPA kufahamu kuhusu sifa za kujiunga kusoma uuguzi, vyuo na ada.
Tandabuhi, Chuo cha mfano Tanzania
Wanafunzi husoma kwa vitendo..
12. Environmental Health
Utaalamu wa mazingira kwa afya. Wataalamu hawa tunawaita mabwana afya.
Kazi yao ni kugundua, kufuatilia na kuchukua hatua kwenye kitu chochote kinachoweza kuleta madhara kiafya katika mazingira.
Fursa zipo nyingi ikiwamo kujiendeleza kimasomo katika fani hii muhimu.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini. Awe na C kwenye masomo 3 ikiwemo Hesabu na kwenye masomo mawili Biologia, Kemia au Physics. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
10. Kozi ya Utunzaji wa taarifa (health management information system):
Katika kila kazi muhimu taarifa muhimu hurekodiwa na kuhifandiwa.
Taarifa hizi huhifadhiwa na wataalamu ili ziweze kupatikana kwa uharaka zinapohitajika na ziwe salama ili kuhakikisha kwamba hakuna uvunjifu wa maadili kama vile kuvujisha siri za za wagonjwa nk.
Taaluma hii humuwezesha mtaalamu huyu kuhifadhi kuumbukumbu kwa mpangilio unaotakiwa na uliokubalika duniani kote.
Takwimu zinapohifadhiwa na kutumika vizuri kuboresha huduma za afya watu wa jamii ile huwa na afya bora.
11. Tabibu wa kinywa na meno (Dentistry)
Madaktari wa meno hujifunza kutunza afya ya kinywa na meno, kuweza kuyachunguza na kuyatibu.
Wako madaktari wa ngazi mbalimbali-diploma, shahada (Doctor Dental Surgery) na daktari bingwa (specialist).
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
Bonyeza HAPA kufahamu zaidi kuhusu kozi ya udaktari wa kinywa na meno
Namna 3 Tunaweza Kukusaidia Utakapokuwa Tayari
CollegePlan tuna plans tatu muhimu zitakazo kuwezesha kufanikisha maombi yako ya vyuo.
- Fahamu inakupa taarifa muhimu za kitaalamu kuhusu kozi na vyuo vya afya ili kukuwezesha kufahamu tofauti ya kozi hizi, sifa za vyuo bora, na kozi inayolipa wakati huu. Bila shaka umegundua hii ni msingi kama siyo lazima
- Fanya inakuwezesha kufanya maamuzi sahihi kuchagua vyuo na kozi kulingana na hali yako halisi. Lengo ni kukupa ushauri mahususi kwa mfano aina ya vyuo kulingana na mahitaji yako ikiwa una mahitaji maalum nk.
- Furahia itakuwezesha huduma zote hadi kuombewa vyuo na kupewa taarifa kuhusu ufadhili ndani na nje ya nchi
Nakushauri usitoke bila plan. Ukishindwa kabisa, chukua Fahamu Plan
Bonyeza Jiunge kuanza na Fahamu. Bonyeza Fahamu kufahamu huduma zetu zingine