Chagua Kozi za Afya za Ndoto Zako

Kozi za afya zimegawanyika katika makundi mawili makubwa:

  1. Masomo ya Kliniki (Clinical): Huusisha uhusiano wa moja kwa moja kati ya mgonjwa na daktari au muuguzi.
  2. Yanayosaidia Matibabu (Allied Health Sciences): Husaidia katika utambuzi na matibabu ya magonjwa.

Usipofahamu makundi haya na vigezo vyake, unaweza kukata tamaa ukifikiri umekosa sifa, au ukachagua kozi isiyoendana na ufaulu wako. Mwaka jana na mwaka huu, kupitia CollegePlan (huduma yetu ya ushauri), tumesaidia wanafunzi zaidi ya 50 waliokuwa wamekosea kuchagua kozi kutokana na kukosa taarifa sahihi.

Kuchagua kozi ya afya ni moja ya maamuzi makubwa zaidi katika maisha ya mwanafunzi. Swali ambalo nimekuwa nikiulizwa kila siku ni: “Je, nina sifa za kujiunga na chuo cha afya?” au “Ni kozi gani ya afya inanilipa?”

Mwongozo huu utakuonyesha orodha ya kozi za afya zinazotolewa nchini, vyuo vinavyofundisha, vigezo vya NACTVET, na ada zao.

Timiza Ndoto Yako ya Afya

Usihangaike peke yako. Pata msaada wa kitaalamu kutoka kwa Dr. Adinan ili ufanikiwe kupata chuo unachokitamani.

BONYEZA HAPA KUPATA MSAADA SASA
  • Soma zaidi: Usiandike Maombi Kimakosa! Pakua ‘Mwongozo wa Udahili 2026’ ujue vyuo vyenye nafasi, sifa zao, na jinsi ya kuomba bila kukataliwa. Bofya Hapa Kupata Nakala Yako

Jedwali la Sifa na Ada za Kozi za Afya kwa ngazi ya diploma 2026

Hapa kuna muhtasari wa haraka wa sifa za kujiunga na vyuo vya afya vya serikali na binafsi. Hii itakusaidia kufahamu kama unakidhi vigezo kabla ya kuanza maombi.

Jina la Kozi (Health Course)Sifa za Kujiunga (CSEE – Kidato cha 4)Muda wa MasomoKadirio la Ada (Tsh / Mwaka)
Clinical Medicine (Utabibu)Alama D ya Bio, Chem, Phys na somo 1 lingine yasiyo ya kidini.Miaka 3 (Diploma)900,000 – 1,200,000
Nursing & Midwifery (Uuguzi)Alama D ya Bio, Chem, Phys na somo 1 lingine.Miaka 3 (Diploma)900,000 – 1,500,000
Environmental Health (Bwana Afya)Alama C ya masomo 3 (ikiwemo Hesabu) na D mbili za Bio, Chem au Phys.Miaka 3 (Diploma)900,000 – 1,200,000
Pharmaceutical Sciences (Famasia)Alama D ya masomo manne (4): Bio, Chem, Phys na somo lingine la kawaida.Miaka 3 (Diploma)1,000,000 – 1,500,000
Medical Laboratory (Maabara)Alama D ya masomo manne (4) ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia.Miaka 3 (Diploma)1,000,000 – 1,400,000
Medical Imaging (Radiolojia)Ufaulu wa Alama D katika masomo matatu (3) ya Sayansi: Kemia, Biolojia, na Fizikia.Miaka 3 (Diploma)1,000,000 – 1,500,000
Physiotherapy (Mazoezi Tiba)Alama D katika masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikijumuisha Kemia, Biolojia na Fizikia.Miaka 3 (Diploma)950,000 – 1,300,000
Occupational Therapy (Tiba Kazi)Ufaulu wa masomo manne (4): Alama C ya Biolojia na D mbili kutoka Kemia, Fizikia, Hesabu au Geo.Miaka 3 (Diploma)900,000 – 1,200,000
Biomedical Engineering (Vifaatiba)Alama D ya masomo manne ya sekondari ikiwemo ufaulu mzuri wa masomo ya Fizikia na Hisabati.Miaka 3 (Diploma)1,100,000 – 1,600,000
Clinical Dentistry (Kinywa & Meno)Alama D ya masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia.Miaka 3 (Diploma)1,000,000 – 1,500,000

Jedwali la Sifa na Ada za Kozi za Afya Ngazi ya Degree 2026

Hapa kuna muhtasari wa haraka wa sifa za kujiunga na vyuo vya afya ngazi ya degree na binafsi. Hii itakusaidia kufahamu kama unakidhi vigezo kabla ya kuanza maombi.

Jina la Kozi (Health Course)Sifa za Kujiunga (ACSEE / Diploma)Muda wa MasomoKadirio la Ada (Tsh / Mwaka)
Doctor of Medicine (MD)Principal Pass 2 (Biolojia na Kemia) – Pointi 4+ za Kidato cha Sita OR Diploma ya G.P.A 3.0+Miaka 5 + 1 (Intern)4,000,000 – 5,200,000
Bachelor of Science in NursingPrincipal mbili za Kemia na Biolojia (Pointi 4) OR Diploma ya Nursing yenye G.P.A ya 3.0+Miaka 3 hadi 41,500,000 – 2,400,000
Bachelor of Environmental HealthUfaulu wa Kidato cha Sita (Kemia na Biolojia) OR Diploma ya Mazingira yenye ufaulu mzuri.Miaka 31,300,000 – 1,800,000
Bachelor of PharmacyPrincipal Pass 2 za Kemia na Biolojia zenye jumla ya pointi 4.0 kutoka ACSEE au Diploma ya Famasia.Miaka 42,000,000 – 3,500,000
BSc in Medical LaboratoryUfaulu wa masomo ya Kemia na Biolojia katika ACSEE OR Diploma ya Maabara (NTA Level 6).Miaka 31,500,000 – 2,200,000

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

Naweza kusoma kozi za afya kama sijafaulu physics?

Kwa kozi nyingi za kitabibu (Nursing, Clinical Medicine), Fizikia ni lazima iwe angalau Alama D. Hata hivyo, baadhi ya kozi za utawala wa afya zinaweza kuwa na vigezo nafuu zaidi.

Timiza Ndoto Yako ya Afya

Usihangaike peke yako. Pata msaada wa kitaalamu kutoka kwa Dr. Adinan ili ufanikiwe kupata chuo unachokitamani.

BONYEZA HAPA KUPATA MSAADA SASA
error: Content is protected !!
Scroll to Top