Vyuo vya Afya Vya Serikali na Binafsi nchini Tanzania

Vyuo vya afya vya serikali vinapendwa zaidi kutokana na ada nafuu na uhakika wa mafunzo. Hapa nimekuandalia orodha ya vyuo vyote vya afya vya serikali na binafsi. Vyuo vya afyavya serikali vimegawanyika katika makundi 2 makubwa. Vyuo vya kati na vya elimu ya juu.

Kama ulikuwa unahitaji kufahamu orodha ya vyuo vya afya vya serikali vilivyopo karibu yako, hapa tutakupatia PdF ya bure. Pia, nitakuonesha namna unaweza kuvifahamu vyuo vyote unapotumia AFYAColleges App.

🔗 Soma pia:Vyuo vya Afya Tanzania (Orodha Kamili na Tofauti Zake)


Vyuo vya Kati vya Serikali (Cheti & Diploma)

Vyuo vya kati vya serikali hutoa mafunzo katika ngazi ya diploma / stashahada na astashahada (certificate). Hii ni orodha ya vyuo vya afya vya kati vya serikali katika baadhi ya mikoa. Unaweza kufahamu orodha kamili kwenye AfyaColleges App.

Jina la ChuoMkoaAina ya Chuo
KCMC Assistant Medical Officers TrainingKilimanjaroSerikali
Mtwara COTCMtwaraSerikali
Mwanza Centre (Lyamungo)MwanzaSerikali
Singida Medical Training CentreSingidaSerikali
Tanga Centre (Bumbuli)TangaSerikali
Mbeya Medical Training CentreMbeyaSerikali
🎓

Usibahatishe Mustakabali Wako!

Kuchagua chuo sahihi ni hatua ya kwanza kuelekea kuwa daktari au nesi mwenye mafanikio. Fahamu vigezo muhimu vya kuzingatia ili usipoteze muda na gharama kwenye chuo kisichokidhi viwango.

FAHAMU JINSI YA KUCHAGUA CHUO BORA

⭐ Mwongozo huu umewasaidia zaidi ya wanafunzi 1,000 mwaka huu.

Vyuo vikuu vya Afya vya Serikali

Vyuo vya juu vya serikali hutoa mafunzo katika ngazi ya shahada (degree), uzamili (masters) na Uzamivu (PhD). Hii ni orodha ya vyuo vya afya vya juu vya serikali katika baadhi ya mikoa. Unaweza kufahamu orodha kamili kwenye AfyaColleges App.

Jina la ChuoMkoaKozi Zitolewazo (Shahada/Degree)
MUHAS (Muhimbili University of Health and Allied Sciences)Dar es SalaamMedicine (MD), Pharmacy, Nursing, Dentistry, Laboratory Sciences, Environmental Health, Physiotherapy, Radiotherapy.
UDOM (University of Dodoma)DodomaMedicine (MD), Nursing, Medical Laboratory Sciences, Health Information Management.
MUST (Mbeya University of Science and Technology)MbeyaBiomedical Engineering, Medical Laboratory Sciences.
SUA (Sokoine University of Agriculture)MorogoroVeterinary Medicine, Biotechnology and Laboratory Sciences.
Mzumbe UniversityMorogoroHealth Systems Management.
OUT (Open University of Tanzania)Nchi NzimaPublic Health, Nursing.
DIT (Dar es Salaam Institute of Technology)Dar es SalaamBachelor of Engineering in Biomedical Engineering.
MoCU (Moshi Co-operative University)KilimanjaroHealth Administration.

Sifa za kujiunga na vyuo vya afya vya serikali kwa ngazi ya diploma 2026

Sifa za kujiunga na vyuo vya afya vya serikali ni kuwa na ufaulu wa D kwa masomo 4 ya sayansi. Fahamu zaidi hapo chini kwenye jedwali. Sifa hizi hutumika pia kwa vyuo binafsi. Kozi za afya hutofautiana sifa za kujiunga.

Jina la Kozi (Health Course)Sifa za Kujiunga (CSEE – Kidato cha 4)Muda wa MasomoKadirio la Ada (Tsh / Mwaka)
Clinical Medicine (Utabibu)Alama D ya Bio, Chem, Phys na somo 1 lingine yasiyo ya kidini. Hisabati na Kiingereza ni sifa ya ziada.Miaka 3 (Diploma)900,000 – 1,200,000
Nursing & Midwifery (Uuguzi)Alama D ya Bio, Chem, Phys na somo 1 lingine. Pasi ya Kiingereza na Hisabati huongeza nafasi.Miaka 3 (Diploma)900,000 – 1,500,000
Environmental Health (Bwana Afya)Alama C ya masomo 3 (ikiwemo Hesabu) na alama D ya masomo mawili kati ya Bio, Chem au Phys.Miaka 3 (Diploma)900,000 – 1,200,000
Pharmaceutical Sciences (Famasia)Alama D ya masomo manne (4): Bio, Chem, Phys na somo lingine la kawaida.Miaka 3 (Diploma)1,000,000 – 1,500,000
Medical Laboratory (Maabara)Alama D ya masomo manne (4) ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia.Miaka 3 (Diploma)1,000,000 – 1,400,000
Medical Imaging (Radiolojia)Ufaulu wa Alama D katika masomo matatu (3) ya Sayansi: Kemia, Biolojia, na Fizikia.Miaka 3 (Diploma)1,000,000 – 1,500,000
Physiotherapy (Mazoezi Tiba)Alama D katika masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikijumuisha Kemia, Biolojia na Fizikia.Miaka 3 (Diploma)950,000 – 1,300,000
Occupational Therapy (Tiba Kazi)Ufaulu wa masomo manne (4): Alama C ya Biolojia na D mbili kutoka Kemia, Fizikia, Hesabu au Jiografia.Miaka 3 (Diploma)900,000 – 1,200,000
Biomedical Engineering (Vifaatiba)Alama D ya masomo manne ya sekondari ikiwemo ufaulu mzuri wa masomo ya Fizikia na Hisabati.Miaka 3 (Diploma)1,100,000 – 1,600,000
Prosthetics & Orthotics (Viungo Bandia)Alama C katika masomo matatu (3) kutoka Fizikia, Kemia, Baiolojia au Hisabati/Masomo ya Uhandisi.Miaka 3 (Diploma)1,200,000 – 1,800,000
Clinical Dentistry (Kinywa & Meno)Alama D ya masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi.Miaka 3 (Diploma)1,000,000 – 1,500,000
Health Information Management (Taarifa)Ufaulu wa masomo manne (4) ya kidato cha nne ikijumuisha masomo ya lugha au takwimu/Hesabu.Miaka 3 (Diploma)850,000 – 1,100,000

Sifa za kujiunga na vyuo vya afya vya serikali Ngazi ya Degree 2026

Hapa kuna muhtasari wa haraka wa sifa za kujiunga na vyuo vya afya ngazi ya degree na binafsi. Hii itakusaidia kufahamu kama unakidhi vigezo kabla ya kuanza maombi.

Jina la Kozi (Health Course)Sifa za Kujiunga (ACSEE / Diploma)Muda wa MasomoKadirio la Ada (Tsh)
Doctor of Medicine (MD)Principal Pass 2 (Biolojia na Kemia) – Pointi 4+Miaka 5 + 1 (Intern)4,000,000 – 5,200,000
Nursing & Midwifery (Uuguzi)Alama D ya Bio, Chem, na Phys/Math/Geo.Miaka 3900,000 – 1,500,000
Environmental HealthAlama C ya masomo 3 (ikiwemo Hesabu).Miaka 3900,000 – 1,200,000
Pharmaceutical Sciences (Famasia)Alama D ya Bio, Chem, na Phys/Math/Geo.Miaka 31,000,000 – 1,500,000
Medical Laboratory (Maabara)Alama D ya Bio, Chem, na Phys/Math/Geo.Miaka 31,000,000 – 1,400,000

error: Content is protected !!
Scroll to Top